ZAIDI ya wadau 95 wameshiriki mkutano wa wadau wa watoto ulioratibiwa na Taasisi ya Anjita Child Development Foundation na Sehemu ya Mipango na Uratibu mkoa wa Pwani.
Mkutano huo umewakutanisha wadau wote wanaofanya kazi na watoto ambapo lengo kuu ni ushiriki wao katika uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto. Wadau walioshiriki katika mkutano huo ni pamoja na NGOs, benki CRDB, NMB, NBC na baadhi ya wafanyabiashara.
TECDEN inashirikiana na Asasi mbalimbali na Serikali katika Mikoa yote 26 Tanzania Bara kuratibu utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) 202½2-2025/26. Mkoa wa Pwani TECDEN inashirikiana na Asasi ya Anjita Development Foundation.
https://www.instagram.com/p/CwpP0Q1tPmt/?utm_source=ig_web_copy_link