WADAU zaidi ya 150 mkoani Shinyanga wamepokea program Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) huku wakielezwa sayansi ya makuzi inayoambatana katika nguzo tano za lishe toshelevu,ulinzi na usalama, ,Afya bora,Malezi yenye mwitikio na fursa za ujifunzaji wa awali.
Wadau hao leo tarehe 20/09/2023 baada ya kushiriki uzinduzi wa programu hiyo mkoani Shinyanga wamepewa elimu juu ya Sayansi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kutoka kwa mtaalamu Andrew Nkunga kutoka taasisi ya Mtandao wa malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto nchini (TECDEN).
https://www.shinyangapressclub.co.tz/2023/09/wadau-shinyanga-waipokea-pjt-mmmam.html